Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali.
1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu
Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka.
Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo.
2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji
Hiki utakitafuna taratibu hususani kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kutafuna utaona kazi unaweza kukisaga kisha weka kwenye jino lenye tatizo.
3. Maji ya uvuguvugu na chumvi
Andaa maji yenye uvuguvugu kikombe kimoja kisha changanya na chumvi kiasi cha kijiko kidogo cha chai halafu tumia maji hayo kusukutua kinywa chako kwa dakika mbili hadi tatu na itakusaidia kutuliza maumivu hayo ya jino.