ZESCO YATWAA UBIGWA LIGI KUU ZAMBIA




Ligi Kuu Zambia imemalizika jana ambapo klabu ya Zesco imetawazwa kuwa Mabingwa wapya nchini humo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Mufulila Wanderes.

Wachezaji wa timu ya Taifa Kenya (Harambee Stars) Jesse Werre , Antony Akumu na David Owino walifanikiwa kuisaidia kuibuka na ushindi huo mnono na kutwaa Ubingwa.

Huku mshambuliji raia wa Kenya, Jesse Were akifunga mabao mawili katika mchezo huo uliowapa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani

Bao la kwanza kwa Zesco lilifungwa na mzawa Chin’gandu.

Helikopta ya Jeshi la Zambia ilitumika kupeleka Kombe Ndola

Artikel Terkait

This Is The Newest Post