Naibu Waziri ataka walimu wasinyimwe fursa za kielimu

Kondoa. Naibu Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella  Manyanya amewataka wakuu wa idara za elimu kutoa nafasi kwa walimu pindi wanapotaka kwenda kujiendeleza kielimu  badala ya kuwanyima fursa zinazojitokeza katika vituo vya kazi.

Manyanya aliyasema leo wilayani Kondoa, Dodoma alipokua akifunga semina kwa walimu wa shule za msingi juu ya mtaala mpya na uimarishaji wa stadi za kusoma, kuandika, na kuhesabu (KKK).

"Imekua tabia ya watu kutumia vyeo kuwanyima walimu kwenda kusoma , kujiendeleza na masomo ya juu , hali ikiwa  vizuri kabisa kuwanyima fursa walimu kutumia nafasi hizo pindi zinapojitoeza." alisema Manyanya

Artikel Terkait